Dada mmoja alikutana na kijana mmoja kwa njia ya facebook na wakapendana hapa mtandaoni.
Baada ya kuchati kwa muda mrefu wakaamua waende kuonana na hatimaye
wakaona na binti kukaribishwa katika chumba alichopanga kijana huyo.
Alipofika akaanza kuhisi kuwa amefanya maamuzi yasiyo sahihi kwenda pale
kwani chumba kilinuka harufu ya pombe na bangi na pia kulikuwa na
vijana wengine wapatao wanne wakiwa wamelewa pale.
wakamwingilia kinguvu dada yule na kisha baada ya kugundua kapoteza
fahamu wakamtupa nje karibu na barabara na dada alipopata fahamu kwa
aibu akaondoka na hakumwambia mtu na kukaa kimya.
Miezi michache baadae akagundua kuwa ni mjamzito na kwa sheria za ile
nchi akatakiwa kufukuzwa katika ile jamii kwani amefanya kosa la
kuiabisha jamii kupata ujauzito bila muda wake muafaka kufikia.
Siku chache baadae ikaja onekana maiti yake ikiwa pembeni ya mji ule katika shamba moja akiwa na karatasi mkononi iliyoandikwa:
" Kwa wadogo zangu miliobaki, mitandao ya kijamii ina faida kubwa na
hasa zake pia... kamwe msiwe wepesi wa kufanya maamuzi na kuja kuwa
wahanga wa matatizo niliyokumbana nayo mimi dada yenu.... Nawapenda
sana"
Sala kwa ajili yako
Mitandao ya kijamii itakupa marafiki watao kupanua mawazo ya kuziboresha
kazi zako na sio watakao kuharibia kazi zako na maisha yako pia.
No comments:
Post a Comment