Laana! Kijana adata na Penzi la Nguruwe huko Sumbawanga….Aamua kuacha Shule baada ya Kunogewa
UNAWEZA
kudhani ni Hekaya za Kusadikika! Lakini ni kisa cha kweli kwamba mama
mzazi amemshitaki polisi mwanawe wa kiume, ambaye ni mwanafunzi wa
kidato cha pili mwenye umri wa miaka 16, kwa kile anachodai amechoshwa
na tabia ya mwanawe ya kufanya mapenzi na nguruwe wao jike mara kwa mara
na hata kujikuta akiacha shule.
Amelalamika akidai kuwa kijana huyo amenogewa `penzi’ la mnyama huyo maarufu hapa kama “kitimoto au noah”, kiasi cha kumfanya aache masomo na kuwa mtoro sugu shuleni.
Nguruwe
huyo jike, inadaiwa anafugwa na familia ya mwanafunzi huyo anayesoma
katika shule moja ya umma ya sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga.
Hayo
yalithibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii mkoani Rukwa,
Sixmund Kibassa aliyemweleza mwandishi wa habari hizi jana kuwa mama
mzazi wa mtoto, ameripoti tukio hilo katika jeshi polisi.
Kibassa
alisifu uamuzi huo, akisema ni mafanikio makubwa yanayotokana na Mpango
Shirikishi wa Kitengo hicho wa kuwarejesha shuleni watoto, ambao ni
watoro sugu.
Alisema
mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) ni miongoni mwa watoro sugu 70
kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari katika Manispaa ya
Sumbawanga, waliorejeshwa hivi karibuni kupitia mpango huo shirikishi wa
kuwarejesha watoro shuleni, unaotekelezwa na Kitengo cha Polisi Jamii
mkoani humo.
Kibassa
alisema wazazi na walezi wenyewe wanafika katika kitengo hicho cha
polisi jamii na kuripoti kuhusu watoto wao ambao wamekatiza masomo.
Alisema
wazazi na walezi hao, wanafichua kwamba watoto wao hao licha ya
kutokwenda shuleni, pia nyumbani hawaonekani na kwamba baadhi yao
wamebainika kutumia muda wao mwingi kunywa pombe vilabuni badala ya
kusoma.
“Ni
juzi tu mama mmoja alinifuata na kuripoti kisa cha mwanawe wa kiume
anayesoma Kidato cha Pili katika shule moja ya sekondari, kwamba licha
ya kuwa mtoro sugu shuleni, lakini pia amekuwa na tabia chafu ya kufanya
mapenzi na nguruwe wao jike mara kwa mara…Nilipomhoji kijana huyo
alikiri kufanya hivyo …basi tulimnasihi,“alieleza.
Kwa
mujibu wa Kibassa, baada ya kumsihi mwanafunzi huyo, alikubali
kuendelea na masomo, ambapo alirejeshwa shuleni kwake na kupokewa na
walimu na wanafunzi wenzake kwa furaha.
Akizungumzia
tukio hilo, Daktari wa Tiba ya Binadamu, Dk Paulo Maiga alisema
mwanadamu kufanya mapenzi na mnyama, kuna madhara makubwa, ikiwemo
kuambukizwa virusi ambavyo vikiingia katika mwiliwa binadamu, kuna
uwezekano mkubwa visiweze kutibiwa.
“Hili
ni tatizo kubwa, madhara yake ni makubwa, huyu nguruwe anaweza kuwa
ameshambuliwa na virusi vya ugonjwa ambao ukiingia na kumshambulia
mwanafunzi huyo, upo uwezekanao mkubwa kusiwepo na